2 Timothy 1:12-17

12 aHii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile.

13 bShika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Al-Masihi Isa. 14 cIlinde ile amana uliyokabidhiwa kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.

15 dUnajua ya kuwa watu wote katika Asia wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na Hermogene.

16 eBwana akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu. 17Badala yake, alipokuwa Rumi, alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata.
Copyright information for SwhKC